Wafikishwa mahakamani kwa kuandanamana
Watu wote wamekanusha mashtaka hayo na kuachiwa kwa dhamana ya shilingi elfu mbili za Kenya kila mmoja ambapo kesi hiyo itatajwa tena tarehe 14 Juni mwaka huu.
Katika hatua nyingine Tume huru ya kuratibu shughuli za polisi imesema itachunguza maafisa polisi wanaotumia nguvu kupita kiasi kuwakabili raia wakati wa maandamano.
Mwenyekiti wa Tume hiyo Johnstone Kavuludi amesema maafisa wa polisi wa usalama barabarani ni miongoni mwa wale watakaofanyiwa tathmini ya utendaji kazi wao.
Kavuludi amewaomba wananchi kutoa ushirikiano ili kuwabaini askari wanaotumia nguvu kunyanyasa raia.
Wakati huo huo Askofu Mkuu wa Kanisa Katoliki la Nyeri, Peter Kairu amesema serikali na viongozi wa upinzani wanatakiwa kufanya mazungumzo ili kutatua mgogoro uliopo kati yao na Tume ya Uchaguzi na Mipaka – IECB.
Akizungumza katika sherehe ya kwanza ya maadhimisho ya mwaka ya Mtakatifu Stephen Askofu Kairu amesema mazungumzo hayo yataisaidia nchi kuwa na amani. = > .
UNGANA NASI FACEBOOK KWA KULIKE PAGE YETU