Miili ya wahamiaji wasio na halali waliokuwa katika boti kuelekea nchini Italia imeendelea kuopolewa ambapo taarifa ya Umoja wa Mataifa inasema
Miili ya wahamiaji wasio na halali waliokuwa katika boti kuelekea nchini Italia imeendelea kuopolewa ambapo taarifa ya Umoja wa Mataifa inasema inasadikiwa wahamiaji wapatao 700 wamekufa katika kipindi cha siku tatu zilizopita katika bahari ya Mediterranean.
Kwa mujibu wa taarifa ya Umoja wa Mataifa boti tatu zilizama katika maeneo ya Kusini mwa Italia Jumatano iliyopita ikiwa na wahamiaji.
Watu walionusurika wameliambia Shirika la Umoja wa Mataifa la Kuwahudumia Wakimbizi -UNHCR kwamba boti zao zilizama zikiwa na wahamiaji wengi.
Ripoti kutoka mashirika ya habari nchini Italia zinasema zaidi ya boti 15 zimekuwa zikisafiri kutoka Libya kila siku katika muda wa siku tano zilizopita.
Wengi wa watu waliowasili hivi karibuni ni raia wa Libya, Eritrea na Somalia wanaokimbia mapigano na umasikini katika nchi zao.
Wiki iliyopita zaidi ya wahamiaji 13,000 wameokolewa katika bahari ya Mediterranean. = > .
UNGANA NASI FACEBOOK KWA KULIKE PAGE YETU