Naibu Spika wa Bunge Dkt. Tulia AcksonNaibu Spika wa Bunge Dkt. Tulia Ackson amelazimika kusitisha shughuli za bunge mjini Dodoma kufuatia wabunge kadhaa kuomba miongozo baada ya Waziri wa Elimu, Sayansi, Teknolojia na Mafunzo ya Ufundi Profesa Joyce Ndalichako kutoa taarifa za kuamriwa kurudi nyumbani zaidi ya wanafunzi Elfu saba wa Chuo Kikuu cha Dodoma- UDOM.
Naibu Spika alifikia hatua hiyo baada ya kutokea kwa hali ya kutoelewana ambapo Wabunge hao walionyesha kutoridhika na taarifa hiyo ya Serikali kuhusiana na suala la Wanafunzi hao.
Wanafunzi hao wanadaiwa kuelekezwa kurejea nyumbani kwa madai kuwa wahadhiri wa Chuo hicho hawaingii kufundisha madarasani.
Awali katika kipindi cha maswali na majibu Naibu Waziri wa Nishati na Madini Dkt. Medard Kalemani amewataka watumiaji wa umeme majumbani kuzingatia matumizi sahihi ya umeme ili kuepuka hasara zinazoweza kuzuilika pindi umeme unapokatwa.
Dkt. Kalemani ametoa kauli hiyo bungeni mjini Dodoma alipokuwa akijibu swali la Mbunge wa Songea Mjini Leonidas Gama.
Naye Naibu Waziri Ofisi ya Waziri Mkuu Sera Bunge Kazi Vijana Ajira na Watu Wenye Ulemavu Dkt. Abdallah Possi amesema serikali inafanya mazungumzo na taasisi zote za serikali ili ziweze kujenga miundombinu rafiki kwa watu wenye ulemavu.
Akijibu maswali yaliyoulizwa kwa Wizara ya Afya Maendeleo ya Jamii Jinsia Wazee na Watoto Naibu Waziri wa wizara hiyo Dkt. Khamis Kigwangala ameitaka jamii kuzingatia ustawi pamoja na ulinzi wa mtoto. = > .
UNGANA NASI FACEBOOK KWA KULIKE PAGE YETU