Takwimu hizo zimebainika kutokana na mashauri yaliyopokelewa na Wasaidizi wa kisheria nchini, ambapo inaonyesha asilimia 23 ya mashauri yaliyopokelewa yalihusu migogoro ya ndoa, huku asilimia 22 ya mashauri yakihusu migogoro ya ardhi.
Mfuko wa msaada wa kisheria uliosajiliwa mwaka 2013 kama mfuko wa kutoa ruzuku kwa mashirika yanayojishughulisha na shughuli za utaoji wa msaada wa kisheria ikiwa pamoja na wanasheria, umebainisha kuwa mchango wa kundi hilo nchini umesaidia sana katika kushughulikia kisheria na kutoa msaada kwa wananchi hususan wa maeneo ya vijijini kutetea haki zao.
Wakizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es salaam Mfuko wa Msaada wa Sheria-LSF limeelezea kuwa upatikanaji wa haki na huduma za kisheria ni tatizo linaloikabili sehemu kubwa ya jamii ya watanzania hasa walio masikini, kutokana na gharama kubwa na kutumia muda mwingi kutafuta huduma hizo, na kwamba mfuko huo utaendelea kupanua wigo wa kazi zinazofanywa na wasaidizi wa kisheria nchini ili kusaidia kundi la wananchi waishio vijijini.
Kwa mujibu wa Mfuko wa Msaada wa Kisheria LSF, kada ya wasaidizi wa kisheria ina watu 4,000 nchini, ambapo kwa mwaka jana pekee zaidi ya watanzania 210,000 wamefikiwa na kuepwa uelewa wa masuala ya kisheria kutoka maeneo mbalimbali nchini.
Inakadiriwa kuwa asilimia 88 ya watanzania hawana uelewa wa masuala ya sheria. = > .
UNGANA NASI FACEBOOK KWA KULIKE PAGE YETU