Preview
Follow us on
Loading...

Wabunge wamegomea kuendelea na kikao cha bunge na kutoka nje,Bila Kujali itikadi zao

=>



Wabunge wa bunge la Jamuhuri ya muungano wa Tanzania bila kujali itikadi ya vyama vyao, leo wamegomea kuendelea na kikao cha bunge na kutoka nje, mara baada ya naibu spika wa bunge Dk. Tulia Akson kuzima hoja ya kufukuzwa chuoni kwa wanafunzi wa diploma wa Chuo Kikuu cha Dodoma (UDOM).

Wakiongea na waandishi wa habari nje ya ukumbi wa bunge mara baada ya bunge kusitisha kikao chake, wabunge Joshua Nassari wa Arumeru Mashariki, Esther Bulaya wa Bunda na Stanslaus Mabula wa Nyamagana, wamepinga hatua ya Naibu Spika kutotaka kuwasikiliza wabunge, ambao ndio wawakilishi wa wananchi.

Mapema leo mara baada ya kipindi cha maswali na majibu bungeni, mbunge wa Arumeru Mashariki Bw. Nassari aliomba muongozo wa spika kuhusu bunge lijadili jambo la dharura kuhusiana na kufukuzwa chuoni kwa wanafunzi wa (UDOM), Naibu Spika akakataa na ndipo wabunge wa upinzani wakasimama kupinga.

Kutokana na hali hiyo, ndipo Naibu Spika akaagiza askari wamemtoe nje mbunge huyo wa Arumeru Mashariki, jambo ambalo halikuungwa mkono na wabunge wengi walioamua kutoka nje na kusababisha lisitishe kikao chake.



Wabunge wamegomea kuendelea na kikao cha bunge

= > .

UNGANA NASI FACEBOOK KWA KULIKE PAGE YETU

=>
Newer Posts Older Posts
© Copyright Mwanaudaku | Designed By Code Nirvana
Back To Top