Akizungumza na waandishi wa habari katika ofisi za tume hiyo, wakati akikabidhi ofisi, katibu mtendaji huyo amesema taarifa hizo zilizobainishwa kutokana na chanzo cha kuaminika ndani ya tume hiyo, si za kweli kwakuwa kwa mujibu wa utendaji wa Tume mwenye mamlaka ya kutoa taarifa rasmi ni yeye katibu mtendaji au mwenyekiti wa Tume na wao hawakutoa taarifa hizo hivyo amewaasa wanahabari kwamba suala hilo limeshapita na kutolewa uamuzi ni vyema wakatumia weledi katika kutafuta habari kutoka katika vyanzo halali.
Profesa Yunus amesema anaunga mkono jitihada zinazofanywa na serikali, na kumtaka waziri kuendeleza jitihada hizo za kuinua ubora wa elimu katika ngazi zote ili kuw ana taifa lenye watu walioelimika na wenye mchango mkubwa katika kuendeleza taifa.
Jumatano tarehe 25/05/2016 serikali ilitangaza uamuzi wake wa kuivunja Tume ya Vyuo Vikuu Tanzania TCU, na kuwapumzisha kazi watendaji wanne wa Tume kutokana na sababu zilizoelezwa katika taarifa ya waziri wa elimu, sayansi na teknolojia kwa vyombo vya habari kuwa ni pamoja na kuwepo kasoro katika udahili wa wanafunzi wasiokidhi vigezo. = > .
UNGANA NASI FACEBOOK KWA KULIKE PAGE YETU