Preview
Follow us on
Loading...

Hukumu ya kesi ya uhalifu wa kivita ya Raisi wa zamani wa Chad Hissene Habre

=>
Hukumu  ya kesi ya uhalifu wa kivita inayomkabili dikteta wa zamani wa Chad Hissene Habre ilitarajiwa  kutolewa leo  Jumatatu.

Waendesha  mashitaka wametaka  kiongozi  huyo  wa  zamani mwenye  umri  wa miaka  73  aliyeiongoza  nchini  hiyo  ya  Afrika  ya  kati kuanzia  mwaka  1982  hadi 1990  ahukumiwe  kifungo  cha maisha.

Kesi  ya  Habre  ilianza katikati  ya  mwaka  jana katika  mahakama  maalum  ya  Afrika, iliyoundwa  mjini Dakar na  Umoja  wa  Afrika  chini  ya  makubaliano na Senegal.
Wachambuzi wa mambo wanasema watu 40,000 waliuwawa  katika  kipindi  cha  utawala wake na kufanyiwa ukatili wa kinyama. = > .

UNGANA NASI FACEBOOK KWA KULIKE PAGE YETU

=>
Newer Posts Older Posts
© Copyright Mwanaudaku | Designed By Code Nirvana
Back To Top