Ugonjwa wa Ukimwi bado ni tishio hapa nchini na unachangia kwa kiasi kikubwa kurudisha nyuma maendeleo ya taifa kutokana na nguvu kazi kubwa ya nchi kuathirika na ugonjwa huo.
Hayo yamefahamika jijini Dar es salaam katika mkutano wa wadau wa utafiti wa viashiria na matokeo ya Ukimwi Tanzania ambapo wamejadili upimaji wa hali Ukimwi nchini kwa mwaka 2016/2017, zoezi linalotarajiwa kuanza mapema mwezi ujao nchi nzima.
Akizungumza katika mkutano huo Mkurugenzi Mkuu wa Ofisi ya Takwimu Tanzania Dk Albina Chuwa amebainisha kwamba tafiti zimeonesha Ukimwi umechangia kwa kiasi kikubwa kudumaza maendeleo ya kiuchumi hapa nchini kutokana na kupotea kwa nguvukazi ya uzalishaji.
Mwakilishi Mkazi wa Shirika lisilo la Kiserikali la watu wa Marekani linaloshughulika na masuala ya Afya – ICAP, Dk. Fernandez Moralles amesisitiza kwamba upimaji wa hali ya Ukimwi nchini Tanzania kwa mwaka 2016/2017 utakuwa wa mafanikio zaidi kutoka na kuwepo vya vifaa vya kisasa, ikilinganishwa na miaka iliyopita. = > .
UNGANA NASI FACEBOOK KWA KULIKE PAGE YETU