Mkutano wa mawaziri wa mambo ya nje wa nchi za umoja huo pia umeitaka serikali ya Congo kupiga hatua madhubuti kuelekea uchaguzi kutokana na mvutano wa kisiasa uliopo, na kusisitizia umuhimu wa kuwepo kwa mazungumzo ya kisiasa kati ya serikali na wadau wote ili kufikia makubaliano ya mpango wa wazi na misingi ya kalenda inayoaminika pamoja na mahitaji ya kifedha kwa ajili ya kuendesha uchaguzi mkuu huo.
Aidha, Umoja wa Ulaya umetoa wito kwa Tume Huru ya Taifa ya Uchaguzi (CENI) kutangaza haraka iwezekanavyo kalenda ya uchaguzi itakayowaruhusu wadau mbalimbali wa kisiasa kutoa maoni juu ya hali ilivyo. = > .
UNGANA NASI FACEBOOK KWA KULIKE PAGE YETU