Preview
Follow us on
Loading...

Dkt.Mipango Philip Mpango amewataka wafanyakazi wa wizara kuacha kufanya kazi kwa mazoea

=>
Waziri wa Fedha na Mipango Dkt. Philip Mpango amewataka wafanyakazi wa wizara hiyo kuacha kufanya kazi kwa mazoea badala yake waisaidie serikali kutimiza malengo yake ya kukusanya kodi ipasavyo na kudhibiti matumizi yasiyo na tija ili kuharakisha maendeleo ya nchi.

Waziri Mpango ametoa wito huo mjini Morogoro wakati akizindua baraza jipya la wafanyakazi wa wizara hiyo.

Amesema jukumu kubwa la wizara hiyo ni kukusanya mapato na kuyasimamia na kuomba ushirikiano kutoka kwa wafanyakazi wote wa wizara hiyo watimize wajibu wao ili kufikia malengo hayo.

Akizungumzia bajeti ya Wizara ya Fedha inayotarajiwa kuwasilishwa bungeni wiki hii Waziri Mpango amesema matumizi ya kawaida yamepunguzwa na fedha nyingi kuelekezwa kwenye miradi ya maendeleo. = > .

UNGANA NASI FACEBOOK KWA KULIKE PAGE YETU

=>
Newer Posts Older Posts
© Copyright Mwanaudaku | Designed By Code Nirvana
Back To Top