Halmashauri ya manispaa ya Ilala jijini dsm limezindua task force ya ukusanyaji wa kodi katika halmashauri hiyo ambapo pia itapambana na wakwepa kodi sugu wakiwemo wamiliki wa majengo lengo likiwa kukusanya billion 85 hadi 100.
Mstahiki meya akizungumza na waandishi wa habari amesema Mkakati huo unalenga kuongeza mapato ya manispaa hiyo ili kuboresha huduma za kijamii katika halmashauri hiyo laikini kuwadhibiti watendaji wasiokuwa waadilifu ambao walikuwa wakishirikiana na wafanyabiashara kukwepa kodi za halmashauri hiyo.
Amesema baadhi ya wamiliki wa majengo hususas katika maeneo ya kariakoo wamekuwa wakidanganya na kukwepa kodi,lakini pia ujenzi wao umekuwa haufuati mkataba wa jiji ikiwemo ujenzi wa meneo ya kupaki magari na badala yake wamegeuza maduka au maeneo ya kuhifadhia bidhaa. = > .
UNGANA NASI FACEBOOK KWA KULIKE PAGE YETU