Jeshi la Polisi kanda Maalum Dsm limefungua jarada na kuwachunguza askari wake wanaotuhumiwa kumtorosha kinara wa kuingiza wahamiaji haramu nchini ambapo juzi kinara huyo aliwaingiza wahamiaji haramu 73 kwa njia ya mashua kutoka mombasa na kumkamata Mtuhumiwa lakini baadae alitoweka katika mazingira ya kutatanisha.
Kamishna wa Polisi Kanda Maalum dsm CP Simon Siro amesema Uchunguzi huo umeanza baada ya kupata taarifa kuwa kinara huyo alilitoweka mikononi mwa polisi wa Kigamboni na kubainisha wazi kuwa waliohusika wakibainika hatua kali zitachukuliwa ikiwemo kufukuzwa kazi na kufikishwa mahakamani.
Aidha Jeshi hilo pia limemtia mbaroni Askari wa jeshi la wananchi -JWTZ -Sajent George Kwisema mkazi wa kibonde maji mbagala baada ya kumkuta na Vipande 13 vya meno ya Tembo vyenye thamani ya shiling milion 198 .
Kufuatia Kuongezeka kwa Uhalifu na matukio ya Katika hatua nyingine Cp Siro amewataka wamiliki wa nyumba wote wanaopangisha kuhakikisha mikataba yote inakuwa na picha za wapangaji ili kuwatambua wapangaji kinyume chake jeshi la polisi litachukua hatua ikiwa mpashijaji hatakuwa na taarifa sahihi za mpangaji.
Katika hatua nyungine jeshi hilo linawashikiria watu watano kwa kumpiga risasi na kumuua mfanyabiashara Wiliam Mroso mkazi wa mbezi Msigani katika baada,aidha jeshi hilo pia limefanikiwa kukamata sukari mifuko 35 ya sukari katika ufukwe wa kigamoni iliyokuwa ikiingizwa kigamboni na kuwashikiria watuhumiwa watatu. = > .
UNGANA NASI FACEBOOK KWA KULIKE PAGE YETU