Preview
Follow us on
Loading...

Wema Sepetu Gari Lake Kupigwa Mnada,Mengi Yaelezwa Soma Hapa

=>

Wema Sepetu ‘Madam’
Na RICHARD BUKOS,
DAR ES SALAAM: Lile gari la kifahari aina ya Range Rover Evogue lenye namba za usajili AEK 101MP la muigizaji Wema Sepetu ‘Madam’, limewekwa kiporo na madalali wa Yono Auction Mart waliokuwa wakiyapiga bei magari yaliyokamatwa kwa makosa mbalimbali na wenyewe kushindwa kuyakomboa.
gari la wema
Gari hilo lenye thamani ya shilingi milioni 200 lilikamatwa maeneo ya Mbezi-Africana jijini Dar likiwa na msala wa kuingizwa nchini kinyume na utaratibu sambamba na kutolipiwa kodi.
Jumatatu iliyopita, paparazi wetu aliyekuwa na taarifa za mnada huo, aliibuka kwenye yadi ya Mamlaka ya Mapato nchini (TRA) iliyopo nyuma ya Jengo la Water Front jijini Dar ambapo ilipotimu saa tano na nusu asubuhi, mnada ulianza rasmi.
Kabla ya kuanza mnada huo matajiri zaidi ya hamsini walianza kuyakagua magari yaliyopo kwenye yadi hiyo ingawa mengi yaliyopigwa mnada yalikuwa katika yadi zingine ikiwemo ile ya Baridi, Mnazi Mmoja.
Baadhi ya matajiri walionekana kulitolea macho gari la Wema huku wengine wakisema kutokana na kukaa yadi kwa takriban mwaka mmoja na kupigwa mvua na jua hadi kufikia kuota majani, linaweza kuwasumbua.

“Hapa tuna utaratibu wetu kwa kupiga mnada magari kwa awamu, lakini hata hivyo mimi siyo msemaji wa ofisi, hebu nenda kamuone ‘inchaji’ wa ofisi hii yule paleee… anayeonekana kwenye kioo yule, kata pale kulia halafu pinda kushoto kaongee naye japo sasa hivi namuona ana wageni,” alisema mfanyakazi huyo.
Paparazi wetu alikwenda kwenye ofisi hiyo na kukaa kwenye foleni ya kumuona inchaji huyo na ilipofika zamu yake, bosi huyo alimwambia amsubiri mapokezi mpaka atakapomuita, jambo ambalo halikufanyika.
Katika mnada huo, magari zaidi ya hamsini yalipigwa mnada ambapo gari aina ya Toyota Vitz yaliuzwa kati ya shilingi milioni 5 na kuendelea, Toyota Coaster (shilingi milioni 40), Toyota Prado (shilingi milioni 17), Benzi (shilingi milioni 20), Toyota Swift (shilingi milioni 5), vichwa vya Skania milioni 40 lakini vyote viliwahiwa na matajiri kabla wengine hawajapanda dau.
= > .

UNGANA NASI FACEBOOK KWA KULIKE PAGE YETU

=>
Newer Posts Older Posts
© Copyright Mwanaudaku | Designed By Code Nirvana
Back To Top