Mbwana Samatta ameendelea kuandika historia barani Ulaya baada ya kufunga kwenye mechi yake ya kwanza ya kimataifa kwa ngazi ya klabu barani Ulaya. Usiku wa Julai 14 Genk ilikuwa inacheza dhidi ya Buducnost Podgorica mchezo wa mtoano kuwania kufuzu kwenye michuano ya Europa League katika msimu huu wa 2016/17.
Pambano hilo limemalizika kwa Genk kuibuka na ushindi wa bao 2-0. Genk walianza kupata goli lao la kwanza dakika ya 17 kwa mkwaju wa penati uliozamishwa wavuni na Neeskens Kebano.
Mbwana Samatta akaihakikishia ushindi timu yake kwa kufunga bao la pili dakika ya 79 kipindi cha pili. Nyota huyo wa Tanzania alipumzishwa dakika ya 88 na nafasi yake ikachukuliwa na Leandro Trossard.
Samatta alianza kwenye kikosi cha kwanza cha kocha Peter Maes akimuweka benchi Nikos Karelis anayehusishwa sana kujiunga na klabu ya Nottingham Forest ya England. Karelis aliingia dakika ya 76 kuchukua nafasi ya Kebano mfungaji wa goli la kwanza.
TAZAMA VIDEO YA SAMATTA
=
>
.
TAZAMA VIDEO YA SAMATTA
UNGANA NASI FACEBOOK KWA KULIKE PAGE YETU