Kiongozi wa Kanisa Katoliki duniani, Papa Francis amepata ajali ya kuanguka ghafla alipokuwa akitembea kuelekea kwenye jukwaa lililoandaliwa kwa ajili ya kuendesha ibada, Czestochowa nchini Poland.
Papa Francis mwenye umri wa miaka 79 alisaidiwa kwa haraka na wasaidizi wake na kufanikiwa kuamka na kuendelea na safari hadi kwenye kiti kilichoandaliwa.
Kwa bahati nzuri, kiongozi huyo wa Kanisa Katoliki alionekana kuwa katika hali yake ya kawaida ambapo aliendelea kuongoza ibada hiyo iliyokuwa ikirushwa moja kwa moja kupitia vituo mbalimbali vya runinga na kuangaliwa na mamilioni ya watu.
Kwa mujibu wa Daily Mail, Papa Francis anasumbuliwa na ugonjwa unaojulikana kama Sciatica, ugonjwa ambao wakati mwingine hushusha maumivu ya ghafla kwenye miguu kutoka mgongoni.
UNGANA NASI FACEBOOK KWA KULIKE PAGE YETU