Preview
Follow us on
Loading...

Machangu: Tunahamia Dodoma

=>

DAR ES SALAAM:Baada ya serikali kutangaza kuamishia office zake Dodoma ”Machangu pia watangaza kuamishia shughuli zao Dodoma,Kama serikali yote inahamia Dodoma kwenye makao makuu ya nchi, ina maana hapa Dar hakutakuwa na maana tena! Wateja wote ni Dodoma sasa sisi tunasubiri nini? Na sisi tunahamia Dodoma,” ndivyo alivyosema dadapoa mmoja anaye fanyia shughuli zake maeneo ya Sinza Afrikasana, Dar.

WASIKIE HAWA
Baadhi ya machungudoa wa eneo hilo la Afrikasana walisema kuwa, baada ya kuona wimbi la watu wanataja Dodoma na wao wamejipanga kuhamia huko kwa kuendeleza biashara hiyo.

“Mimi mfano, natokea Tanga, nimekuja Dar kwa ajili ya kujiuza, sasa serikali inapohamia Dodoma maana yake ni kwamba, mambo mengi, yatahamia kule. “Nimesikia watu wakisema kuwa, hapa Dar patabaki peupe kwani hata foleni zitakwisha, msongamano utakuwa Dodoma.
Sasa mimi Dar nabaki kufanya nini?” alisema mmoja wa machangu hao akisema anaitwa Mwajabu Idi, mkazi wa Mapinduzi, Tanga. Mwenzake aliyedai anaitwa Kidawa, mkazi wa Morogoro alisema: “Kwenda Dodoma si hiari yetu bali ni hali halisi. Kazi yetu (ya kuuza miili) haina tofauti na wafanyabiashara wengine, unaangalia soko liko wapi? Kwa hiyo kama soko litahamia Dodoma na sisi hukohuko.”

HALI YA DODOMA KWA SASA
 Tangu Rais Dk.
John Pombe Magufuli ‘JPM’ atangaze kwenye Mkutano Mkuu wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) kwamba, ndani ya miaka minne na miezi minne iliyobaki ya utawala wake, serikali yote itahamia Dodoma, mji huo umebadilika ghafla.
“Na si kwa tangazo la Magufuli tu. Hata Waziri Mkuu Kassim Majaliwa alipotangaza kwenye maadhimisho ya Siku ya Mashujaa, Julai 25 hapa mjini Dodoma kwamba yeye atakuwa wa kwanza kuhamia Dodoma Septemba mwaka huu, hali kwenye mji huu imebadilika.
“Baadhi ya wenye nyumba wameanza kupandisha bei ya vyumba, nyumba. Wenye viwanja nao bei juu. Lakini matajiri wenye hoteli nao wameanza kukarabati wakijua wanaingia kwenye ushindani wa kibiashara,” alisema mkazi mmoja wa mji huo aliyejitambulisha kwa jina la Msokola.

WAFANYABIASHARA WA DAR
Sambamba na hali hiyo, wafanyabiashara wengi wa jijini Dar es Salaam wameanza kujipanga kwa uwekezaji mkubwa utakaofanyika mjini Dodoma.
“Unajua awamu zote zilisema zitahamia Dodoma. Alianza Baba wa Taifa (Julius Nyerere), akaja Mzee Ruksa (Ali Hassan Mwinyi), akaja mzee Mkapa (Benjamin) na hata JK (Jakaya Kikwete).
“Lakini hakuna aliyefanikisha.
Sasa huyu JPM bwana hanaga utani wala kusubiri. Akisema amesema, najua kweli atahamia Dodoma, we utaona. Ndiyo maana hata sisi wafanyabiashara tunajipanga kwenda Dodoma,” alisema Alex Shayo, mfanyabiashara wa baa, Kimara.
= > .

UNGANA NASI FACEBOOK KWA KULIKE PAGE YETU

=>
Newer Posts Older Posts
© Copyright Mwanaudaku | Designed By Code Nirvana
Back To Top