Preview
Follow us on
Loading...

Kauli Ya Zitto Kabwe Uenyekiti Wa Magufuli CCM

=>

Rais wa Tanzania Dkt.John Pombe Magufuli pamoja na Zitto Kabwe.
Rais wa Tanzania Dkt.John Pombe Magufuli pamoja na Zitto Kabwe.

Mbunge wa Kigoma mjini Zitto Kabwe kupitia account yake ya facebook amempongeza Rais Dkt.John Pombe Magufuli kukabidhiwa uenyekiti wa Chama cha Mapinduzi (CCM) kwa kupata  kura zote  za ndio 2398.
Huu ndio ujumbe wake,
“Napenda kumpongeza Rais John Magufuli kwa kuchaguliwa kwake kuwa Kiongozi wa Chama chake cha CCM akiwa Mwenyekiti wa Tano chama hicho. CCM imeendelea kudumisha utamaduni wa kukabidhiana Uongozi kila baada ya muda
“Jambo ambalo ni la kujifunza hasa kwa vyama vya Siasa nchini na barani Afrika. Nataraji kwamba Rais na Mwenyekiti mpya wa CCM ataona umuhimu wa Vyama vya Siasa kuendelea kufanya Siasa bila vikwazo na kwa mujibu wa Sheria za Nchi yetu.
“Demokrasia inaimarisha Amani kwa kupaza sauti za HAKI. Karibu kwenye changamoto za kuongoza Vyama vya Siasa ndugu Rais.” –Zitto Kabwe
= > .

UNGANA NASI FACEBOOK KWA KULIKE PAGE YETU

=>
Newer Posts Older Posts
© Copyright Mwanaudaku | Designed By Code Nirvana
Back To Top