Preview
Follow us on
Loading...

Gigy Money, Idris mahaba niue!

=>

IMEVUJA! Baada ya hivi karibuni penzi la Wema Sepetu na Idris kusambaratika, mwanadada Gift Stanford ‘Gigy Money’ amedaiwa kuchukua nafasi na sasa ni mapenzi motomoto.
Chanzo makini,mwanadada huyo aliamua kutafuta kazi ya utangazaji kwenye Kituo cha Redio cha Choice FM ili amnase Idris ambaye naye ni mtangazaji wa hapo.
Alimfuata Choice (Choice FM) ili amnase vizuri na kweli amefanikiwa na hata kuachana kwa Idris na Wema kuna chembechembe za yeye kulivuruga penzi lao kwani baada ya kuachana ndiyo mapenzi yamekuwa motomoto sana,” Hivi karibuni Gigy Money alitundika picha kwenye ukurasa wake wa mtandao wa kijamii wa Instagram akiwa na Idris huku akisindikizia na maneno kwamba ‘Hainaga ushemeji tunakulaga, leo niweke wazi kabisa jamani huyu ni mume wangu’.
Baada ya kupata habari hizo, Mwanaudaku tuliamua kumtafuta Gigy Money ili kuupata ukweli ambapo alikuwa na haya ya kusema;
“Idris ameachana na Wema na nilijitahidi kutafuta kazi kwenye redio Choice ili niweze kumnasa vizuri na kweli nimefanikiwa, kiukweli nimejikuta nampenda sana. Sioni tatizo yeye ni mwanaume, mimi ni mwanamke, acha maisha yaendelee,” alisema Gigy.
Jitihada za kumpata Idris aweze kuzungumzia penzi hilo hazikuzaa matunda kufuatia simu yake ya mkononi kuita bila kupokelewa.
= > .

UNGANA NASI FACEBOOK KWA KULIKE PAGE YETU

=>
Newer Posts Older Posts
© Copyright Mwanaudaku | Designed By Code Nirvana
Back To Top