Chama Cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), leo kimepiga hodi Mahakama ya Afrika Mashariki, Jijini Arusha na kuishitaki Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kwa kile kinachodaiwa kuwa uvunjwaji wa vipengele muhimu vya Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania. katika kuikandamiza demokrasia.
Kesi hiyo imefunguliwa na Mwenyekiti wa Chadema, Freeman Mbowe Naibu Katibu Mkuu wa Chadema, John Mnyika kupitia kwa Mwanasheria wa chama hicho, John Malya ikiishitaki Serikali juu ya unyanyasaji wa Bunge la Tanzania kwa wapinzani na kuzuiliwa kwa mikutano ya kisiasa kinyume na katiba.
Walalamikaji wengine katika kesi hiyo ni wanachama wa Chadema huku wajibu mashtaka wakiwa ni Mwanasheria Mkuu wa Serikali na Katibu Mkuu wa Jumuiya ya Afrika Mashariki.
Hatua hii ya Chadema inakuja baada ya kugonga mwamba katika Shauri lililofunguliwa Mahakama Kuu Kanda ya Mwanza kuhusiana na maswala kama haya huku wabunge wa upinzani wakiwa wamesusia vikao vya bunge kwa muda mrefu sana hadi kupelekea kulikosa bunge lote la bajeti kwa kile kinachodaiwa kuwa ni kukandamizwa na Naibu Spika, Dkt. Tulia Ackson aliyeendesha vikao vya vyote vya bunge ambavyo wabunge wa upinzani wamevisusia.
UNGANA NASI FACEBOOK KWA KULIKE PAGE YETU