Wakiwa kwenye mkutano wa Mtaa wakimtaja mwekezaji huyo kwa jina moja na Saimoni anayedaiwa kuwa na asili ya Kenya ,wananchi hawa wanasema wamefikia uamuzi huo baada ya kuona ni muda mrefu sasa, hakuna hatua zozote za ujenzi katika eneo hilo, wakati mwekezaji huyo aliahidi kujenga shule katika kipindi cha miaka mitatu tangu kukabidhiwa mwaka 2003, na badala yake amekuwa akitumia eneo hilo kukodishia wananchi kulima mazao mbalimbali.
Kutokana na hali hii wananachi hawa wameamua kuchukua eneo hilo na kulitumia kwa matumizi yao .
Channel Ten imemtafuta mwekezaji huyo kwa njia ya simu na katika maelezo yake amedai yuko nje ya Mkoa wa Mbeya nakwamba akirejea atolea ufafanuzi suala hilo. = > .
UNGANA NASI FACEBOOK KWA KULIKE PAGE YETU