Wakati nafunga mlango wa room nashtuka kumuona mke Wa Rafiki yangu akitoka Chumba mkabala na changu akiongozana na zee moja hivi nao wakifunga Chumba chao shemeji alitetemeka na kupata mshtuko mkubwa hadi yule Mzee kumuuliza kuna nini
Mchepuko wangu ulishatangulia kwenye gari nikamsalimia shemeji nikamwambia mm ndo na check out nilikua semina ya siku tatu ndo imeisha, akaitikia kwa kichwa tu,
Nikapiga hatua za haraka kwenda kwenye Gari ili asiuone mchepuko wangu ambao ulishatangulia kwenye gari
Jumatatu akanipigia simu mwenyewe akaniambia shemeji naomba unifichie siri sitarudia tenaNikamwambia naomba tuongee baadae kwa sasa nipo busyMchana wake akanitumia meseji inasomeka hivi "" Shem naomba kama vipi tafuta sehemu nije tumalizane kiutu uzima and you stay silence forever "" naomba unijibu i can't afford to loose this marriage
Wakuu nipo njia panda, ingawa mm ni mzinzi na sina utakatifu lakini siwezi kutembea na mke Wa Rafiki yangu kipenzi tulieshibana miaka nenda miaka Rudi
Na nilishawahi kukaa kwake sana wakati sijapata kazi yy alianza kuja dar kabla yangu
Kwa sasa huyu jamaa yupo mkoani kikazi alihamishiwa huko mke alishindwa kumfuata kwa yy mwenyewe ana kazi hapa dar .Jana kanitumia M-PESA laki tano ikisindikizwa na msg kuwa vipi shemeji lile suala letu umeamuaje ukimya wako unaniumiza.
Sikujibu kitu
Wakuu naomba muongozo wenuKweli nisimwambie Rafiki yangu kuhusu uzinzi Wa mkewe?Na mm ndo nimepewa jukumu la kumuangalizia familia yake kwa mambo mbali mbali kwa kuwa yupo mbali
Nawasikiliza wakuu = > .
UNGANA NASI FACEBOOK KWA KULIKE PAGE YETU